Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 10:24

Wahouthi waendelea na mashambulizi bahari ya Sham

Shambulizi la ndege zisizo na rubani liliharibu meli ya wafanyabiashara katika bahari ya Sham karibu na Yemen Jumapili, mashirika mawili ya usalama wa baharini yamesema, wakati waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran wakitangaza mashambulizi ya baharini katika njia muhimu kwa biashara.

Meli za ndani na karibu na bahari ya Sham zimekuwa zikishambuliwa mara kwa mara kwa miezi kadhaa na waasi wa Houthi wa Yemen.

Wanasema kuwa wanaunga mkono Wapalestina wakati kwa vita vya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Shambulizi la karibuni limetokea takriban kilomita 120 magharibi mwa mji wa bandari wa Yemen wa Hodeida, imesema Operesheni za Biashara za Baharini ya Uingereza (UKMTO), ambayo inaendeshwa na Jeshi la Wanamaji la Uingereza.

Forum

XS
SM
MD
LG