Meli hiyo ilitoa taarifa kwa njia ya redia kwenye ufukwe wa mji wa bandari unaoshikiliwa na waasi wa Hodeida ikisema kuwa imeshambuliwa.
Hayo ni kwa mujibu wa kampuni binafsi ya usalama ya Ambrey, ambayo iliongeza kuwa meli ya kivita katika eneo hilo ilijibu mashambulizi hayo.
Kituo cha Operesheni za Biashara za Baharini cha Uingereza cha jeshi la Uingereza baadaye pia kiliripoti mashambulizi hayo, kikisema kuwa maafisa wa jeshi katika eneo hilo walikuwa wakifanya uchunguzi.
Baadaye wapiganaji wa Kihouthi walidai kuhusika na shambulio hilo, na kuitaja kuwa ni Seajoy na ambapo wamesema walitumia bodi isiyo na nahodha kufanya mashambulizi hayo.
Forum