Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 09:37

Vita vya Gaza vinaweza kusambaa


Maafisa wa Marekani na Ulaya wanatahadharisha juu ya uwezekano wa vita vya Gaza kusambaa, huku kukiwa na matarajio ya mashambulizi ya Israel nchini Lebanon, dhidi ya kundi la wanamgambo wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, amewaambia waandishi wa habari Jumatatu, Luxembourg kwamba hatari ya vita kusambaa inaongezeka kila siku.

“Nadhani, kwa bahati mbaya tuko katika kipindi ambacho vita vinaweza kusambaa,” Borrell amesema.

Pia amesema kusitishwa kwa mapigano ya Gaza kunahitajika sana kuwezesha usambazwaji wa misaada ya kibinadamu, akisema uwasilishaji wa misaada ya kibinadamu ndani ya Gaza hauwezekani.

Gati la muda ambalo lilijengwa kwa ajili ya misaada ya Gaza kupitia njia ya baharini lilisitisha usafirishaji Jumatatu kutokana na matengenezo, msemaji wa Pentagon, Meja Jenerali Pat Ryder aliwaambia waandishi wa habari.

Forum

XS
SM
MD
LG