Kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran limekuwa likishambuliana na Israel, tangu kuzuka kwa vita vya Gaza miezi 8 iliopita, likisema kuwa halitasitisha mashambulizi hadi pale kutakapokuwa na sitisho la mapigano huko Gaza.
Kabla ya kuanza safari yake ya Washingon, Gallant kupitia taarifa amesema kwamba wapo tayari kwa hatua yoyote inayohitajika huko Gaza, Lebanon na maeneo mengine. Mapema mwezi huu Hezbollah walilenga miji kadhaa ya Israel, pamoja na vituo vya kijeshi, baada ya Israel kuuwa kamanda wa ngazi ya juu zaidi wa kundi hilo.
Mjumbe wa Marekani Amos Hochstein wiki iliopita alitembelea Lebanon na Israel, akijaribu kupunguza mzozo uliopo kwenye mpaka wa mataifa hayo. Baadhi ya maafisa wa Israel wameashiria kuwa huenda Israel ikalenga Lebanon, baada ya mashambulizi ya mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah yanayosemekana kulenga kundi la mwisho la wapiganaji wa Hamas.
Forum