Tishio la vita vikubwa kwenye mpaka wa kaskazini wa Israel liligusiwa Alhamisi katika mazungumzo mjini Washington, ambapo waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na mshauri wa usalama wa taifa wa White House Jake Sullivan, walikutana na mshauri wa usalama wa taifa wa Israel Tzachi Hanegbi na waziri wa masuala ya mkakati Ron Dermer.
Majadiliano yao yalizungumzia pia juhudi za kufikia sitisho la mapigano huko Gaza, kuhakikisha kuachiliwa kwa mateka wote ambao bado wanashikiliwa na Hamas, na kuongeza misaada ya kibinadamu kwa raia wa Palestina.
“Tumekuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya kaskazini mwa Israel,” msemaji wa wizara ya mambo ya nje Matthew Miller aliwambia waandishi wa habari Alhamisi.
“Tumeshuhudia ongezeko kubwa la mashambulizi ya Hezbollah kwenye mpaka yanayolenga vijiji vya Israel, makazi ya raia. Na kwa hiyo, tunatafuta njia ya kidiplomasia kujaribu kueleza wazi kwamba hakupaswi kuwa ongezeko la mapigano.”
Forum