Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 08, 2024 Local time: 10:37

Wapalestina wawatafuta wenzao katika vifusi


Uharibifu wa majengo katika Eneo lililoko mpakani kati ya Misri na Ukanda wa Gaza , Julai 4 2924. Picha na Giuseppe CACACE / AFP.
Uharibifu wa majengo katika Eneo lililoko mpakani kati ya Misri na Ukanda wa Gaza , Julai 4 2924. Picha na Giuseppe CACACE / AFP.

Wapalestina walikuwa wakitafuta watu na vitu vyao kwenye vifusi huko Gaza katika mji wa Khan Younis hivi leo kufuatia shambulizi la Israel karibu na shule ya inayoendeshwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wasiokuwa na makazi.

Shambulizi lilitokea wakati kukiwa na wito wa kuanza tena kwa harakati za sitisho la mapigano kati ya Israel na hamas katika miezi tisa ya vita huko Ukanda wa Gaza.

Baada ya wiki kadhaa kukiwa na harakati chache za kidiplomasia, wapatanishi wa Misri na Qatar waliwasilisha majibu kutoka Hamas kwa pendekezo ambalo litajumuisha kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa huko Gaza na sitisho la mapigano katika eneo la Palestina.

Israel inauangalia waraka huo, na imesema katika taarifa yake iliyotolewa na ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwa niaba ya idara ya kijasusi ya Mossad.

Mustafa Al Attal, amabye nyumba yake iliharibiwa katika shambulizi la anga alielezea mashaka yake kuhusu makubaliano hayo.

“tunasikia kwamba kutakuwa na maridhiano na kutakuwa na hili ama lile. Lakini yote hayo hayana chochote. Netanyahu hataki chochote,” amesema wakati akiwa anachakura kwenye mlima wa vifusi.

Forum

XS
SM
MD
LG