Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 22:58

Israel yatoa amri ya kuwahamisha Wapalestina Khan Younis


Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Israel ilitoa Amri ya kuwahamisha Wapalestina katika baadhi ya maeneo ya Khan Younis na maeneo jirani, amri ambayo huenda inaashiria Israel inapanga kuushambulia tena mji huo wa kusini mwa Gaza.

“Inaonyesha kwa mara nyingine kwamba hakuna mahali salama huko Gaza, juhudi zaidi zinahitajika kulinda raia,” msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Stephane Dujarric alisema.

Mkazi ambaye anaishi katika eneo ambako watu watahamishwa, Ahmad Najjar, ameiambia AFP, “ Woga na wasiwasi mkubwa umewakumba watu baada ya amri ya kuhama.” Amesema aliona idadi kubwa ya wakazi wakihama.

Amri hiyo ya kuwahamisha watu inajiri wakati kukiwa taarifa kwamba Israel ilimuachia huru mkurugenzi wa hospitali kuu ya Gaza Jumatatu kama sehemu ya kuachiliwa kwa Wapalestina kadhaa ambao walirejea Gaza kwa ajili ya kupewa matibabu.

Mohammed Abu Selmia amekuwa akizuiliwa tangu mwezi Novemba. Aliongoza hospitali ya Shifa huko Gaza ambayo ilivamiwa na wanajeshi wa Israel mwezi huo huo, huku wakidai kwamba wanamgambo wa Hamas walikuwa wakitumia kituo hicho kama kamandi yao.

Forum

XS
SM
MD
LG