Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 10:27

Isreal inaendelea na mashambulizi Ukanda wa Gaza, imeagiza raia kuondoka


Wapalestina waliokoseshwa makao mashariki mwa Khan Yunis July 2, 2024
Wapalestina waliokoseshwa makao mashariki mwa Khan Yunis July 2, 2024

Wanajeshi wa Israel wametekeleza mashambulizi katikati na kusini mwa ukanda wa Gaza huku wapalestina wakitafuta sehemu zingine za kukaa baada ya Israel kutoa amri ya kuwataka kuondoka.

Jeshi la Israel limesema kwamba limelenga wanamgambo wa Hamas kwa mashambulizi ya angani, katika mji wa Rafah.

Oparesheni ya ardhini inaendelea katika wilaya ya Shujaiya, Gaza City, kaskazini mwa Gaza.

Umoja wa mataifa umeeleza wasiwasi mkubwa kuhusu amri ya Israel ya kutaka wakaazi kuondoka sehemu kubwa ya kusini mwa ukanda wa Gaza.

Umoja wa mataifa umesema kwamba hatua hiyo itawaathiri maelfu ya raia.

Forum

XS
SM
MD
LG