Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 03:21

Mkurugenzi wa Idara ya Secret Service Marekani ajiuzulu


Kimberly Cheatle
Kimberly Cheatle

Mkurugenzi wa idara ya ulinzi wa viongozi (Secret Service), Kimberly Cheatle, amejiuzulu leo Jumanne, siku moja baada ya kukiri kuwa idara hiyo ilishindwa katika dhamira yake ya kuzuia jaribio la mauaji dhidi ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.

Cheatle alikuwa akikabiliwa na wito wa pande mbili kujiuzulu baada ya mtu mwenye bunduki, mwenye umri wa miaka 20 kumjeruhi Trump, Mrepublican na mgombea wa sasa wa urais, katika mkutano wa kampeni wa Julai 13 mjini Butler, Pennsylvania.

"Alikuwa amechelewa, alipaswa kufanya hivi takriban wiki moja iliyopita," Mike Johnson, Spika Mrepublican wa Baraza la Wawakilishi, aliwaambia waandishi wa habari. "Nina furaha kuona kwamba ametii wito wa Warepublican na Wademocrat."

Cheatle alifika mbele ya kamati ya bunge siku ya Jumatatu na kusema kuwa shambulizi dhidi ya Trump, ambaye alijeruhiwa kidogo kwenye sikio lake la kulia, liliwakilisha kushindwa kwa idara hiyo ya Secret Service.

Warepublican na Wademokrat walimtaka Cheatle ajiuzulu. Aliwakasirisha wabunge kutoka pande zote mbili kwa kukataa kutoa maelezo mahsusi kuhusu shambulio hilo, akitoa mfano wa kuwepo kwa uchunguzi unaoendelea.

Mshambuliaji huyo alimfyatulia risasi Trump kwa bunduki aina ya AR dakika chache baada ya kuanza kuwahutubia waliohudhuria hafla hiyo ya kampeni.

Akiwa juu ya paa la jengo lililo karibu, aliuawa kwa kupigwa risasi na afisa wa Secret Service chini ya sekunde 30 baada ya kufyatua risasi ya kwanza, kati ya nane zilizotumika.

Forum

XS
SM
MD
LG