Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 20:21

FBI waingia nyumbani kwa mshukiwa aliyempiga risasi Trump


Maafisa wa FBI wakiingia nyumbani kwa mshukiwa aliyempiga risasi Trump Julai 15 huko Bethel Park, Pennsylvania Julai 15, 2024. Picha na Reuters
Maafisa wa FBI wakiingia nyumbani kwa mshukiwa aliyempiga risasi Trump Julai 15 huko Bethel Park, Pennsylvania Julai 15, 2024. Picha na Reuters

Maafisa wawili wa FBI siku ya Jumatatu wameonekana wakiingia nyumbani kwa mshukiwa aliyempiga risasi rais wa zamani Donald Trump.

Azma ya mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 20 Thomas Matthew Crooks bado ni kitendawili siku mbili badaye, mshukiwa huyo alipigwa risasi na kufa. FBI haikuweza kufahamu itikadi ambayo huenda ilimsukuma kumshamulia rais wa zamani.

FBI wanaongoza uchunguzi wa shambulio hilo la risasi katika mkutano wa hadhara huko Pennsylvania ambako rais wa zamani alijeruhiwa. Ikifunika uchaguzi wake wa Novemba 5 anapochuana tena na Rais Joe Biden.

Biden aliamuru tathmini huru kuona jinsi mshukiwa huyo ambaye aliuawa muda mfupi baada ya kufyatua risasi, kama angekuwa karibu sana angeweza kumuua au kumjeruhi vibaya Trump licha ya ulinzi mkali uliotolewa na Secret Service siku ya Jumamosi (Julai 13) katika kampeni huko Butler, Pennsylvania.

Taarifa za awali kuhusiana na uchunguzi wa mshukiwa aliyekuwa na silaha Thomas Matthew Crooks, alikuwa akifanya kazi katika nyumba ya wauguzi, hazina maelezo ya kina.

Alikuwa kijana, aliyeanza kazi katika mji anaoishi wa Bethel Park, Pennsylvania. Alihitimu masomo ya sekondari mwaka 2022 akiwa na sifa ya kuwa mwanafunzi mwenye akili sana. Mshauri wake alimuelezea kuwa “alikuwa na heshima” na hakujua kabisa Crooks kuwa katika siasa.

Forum

XS
SM
MD
LG