Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 18:41

Vijana wakusanyika Nairobi kuwakumbuka wenzao waliokufa kwenye maandamano


Mwandamanaji akitorokea gesi ya kutoa machozi, wakati wa maandamano ya Nairobi.
Mwandamanaji akitorokea gesi ya kutoa machozi, wakati wa maandamano ya Nairobi.

Mamia ya wakenya Jumapili wamekusanyika kwenye mji mkuu Nairobi, kuhudhuria hafla ya kumbukumbu ya zaidi ya darzeni 3 ya watu waliokufa kwenye maandamano ya kupinga serikali ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, takriban watu 39 walikufa kwenye maandamano hayo yalioanza Juni 18, yakipinga mswaada wa bajeti ambao ungeongeza kodi, huku baadhi pia wakiitisha kujiuzulu kwa rais William Ruto.

Mwanaharakati wa haki za kijamii Boniface Mwangi wakati akizungumza na Reuters amesema kuwa,” Licha ya huzuni iliopo, wanafurahi kuona kwamba serikali inasikiliza wananchi kutokana na maandamano hayo.”

Kwenye hafla hiyo ambayo imefanyikia kwenye bustani ya Uhuru, vijana walionekana wakiwa wameshika mabango yenye maneno na picha za kuwaenzi wenzao waliofariki.

Hilo limefanyika Julai 7 tarehe ambayo inaibua kumbukumbu za mwaka 1990, ambapo maandamano sawa na hayo yalianza na kulazimisha serikali ya rais Daniel Arap Moi kuruhusu siasa za vyama vingi.

Forum

XS
SM
MD
LG