Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 21:43

Jinsi vita Gaza inavyo sababisha vifo vya watoto kutokana na utapiamlo na ukosefu wa matibabu


Mama wa Kipalestina Ghaneyma Joma akiwa na mtoto wake Younis Joma ambaye afya yake imeendelea kuwa mbaya kutokana na vita, katika hospitali ya Nasser, huko Khan Younis, upande wa kusini wa Ukanda wa Gaza, Julai 8, 2024. REUTERS/Mohammed Salem
Mama wa Kipalestina Ghaneyma Joma akiwa na mtoto wake Younis Joma ambaye afya yake imeendelea kuwa mbaya kutokana na vita, katika hospitali ya Nasser, huko Khan Younis, upande wa kusini wa Ukanda wa Gaza, Julai 8, 2024. REUTERS/Mohammed Salem

Mama wa Kipalestina Ghaneyma Joma alikuwa amekaa chini katika hospitali ya Nasser huko Khan Younis, Gaza, akiwa na mtoto wake wa kiume Younis Joma ambaye afya yake imeendelea kuwa mbaya tangu kuanza kwa vita, alisema.

“Inahuzunisha kumuona mtoto wangu mbele ya macho yangu akisubiri kufa kutokana na utapiamlo kwa sababu siwezi kumpatia kitu chochote kutokana na vita, kufungwa kwa vivuko na maji machafu,” alisema.

Younis ni mmoja wa watoto wa Kipalestina ambao wanaguswa na athari za vita huku kukiwa na uhaba wa chakula na maji safi.

Hospitali pia zinakabiliwa na idadi kubwa ya wagonjwa na huku huduma zikiwa finyu kutokana na vita.

Daktari wa watoto, Mervat Al-Qatati, alisema Hospitali ya Nasser haiwezi kutoa matibabu kwa mmiminiko mkubwa wa wagonjwa watoto ambao wanawapokea.

Kampeni ya Jeshi la Israel imeziweka hospitali nyingi na vituo vingine vya afya kushindwa kutoa huduma, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), na kusababisha uhaba mkubwa wa mahitaji ya tiba.

Israel inakanusha kuw akwa makusudi inavilenga vituo vya afya au kuzuia upatikanaji wa mahitaji ya tiba kufika Gaza.

Younis Joma ambaye afya yake imeendelea kuwa mbaya kutokana na vita.
Younis Joma ambaye afya yake imeendelea kuwa mbaya kutokana na vita.

Vita vilianza Oktoba 7 wakati wapiganaji kutoka kundi la wanamgmabo wa Palsetina Hamas walipovamia mpakani na kuzishambulia jamii mbalimbali huko Israel, na kuua watu 1,200 na kuwateka watu 250, kulingana na idadi iliyotolewa na Israeli.

Shambulizi la Israeli huko Gaza ni majibu ambayo yalianza siku hiyo hiyo kwa mashambulizi ya mabomu na yameendelea kwa miezi tisa pamoja na uvamizi wa ardhini ambapo mamlaka za afya Palestina zinasema yameuwa zaidi ya watu 38,000 na kujeruhi zaidi ya watu 80,000.

Idadi kubwa ya waliojeruhiwa kutokana na vita hivyo imeongeza magonjwa kusambaa na utapiamlo miongoni mwa asilimia 90 ya wakazi wa Gaza ambapo Umoja wa Mataifa unasema wamekoseshwa makazi, na kuweka shinikizo kubwa kwa mfumo wa afya katika eneo hilo finyu.

Forum

XS
SM
MD
LG