Mabadiliko hayo yanajiri wakati Misri inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo vita vya Gaza kwenye mpaka wake, matatizo ya uchumi na ukosefu wa umeme.
Wakati baraza la mawaziri la awali lilopojiuzulu mwezi mmoja uliopita, Sisi alimteua tena waziri mkuu Mostafa Madbouly na kusema kwamba serikali yake mpya inastahili kuangazia namna ya kupunguza mfumuko wa bei na kudhibiti masoko pamoja na kuimarisha uwekezaji.
Ahmed Kouchouk ameapishwa kuwa waziri wa fedha. Alikuwa naibu wa waziri wa fedha. Anakabiliwa na changamoto kubwa sana ikiwemo uchumi unaodorora na mzigo mkubwa wa deni la serikali ambalo limekuwa likiongezeka katika miaka ya hivi karibuni.
Mawaziri wa Misri wana mamlaka madogo ya kufanya maamuzi. Nguvu zipo mikononi mwa rais, jeshi na huduma ya usalama.
Forum