Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 09:59

Chama cha waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak chashindwa vibaya katika uchaguzi wa bunge


Kiongozi wa Chana Cha Labor, Keir Starmer akifanya kampeni huko Redditch Worcestershir, Julai 3, 2024. Picha na Reuters.
Kiongozi wa Chana Cha Labor, Keir Starmer akifanya kampeni huko Redditch Worcestershir, Julai 3, 2024. Picha na Reuters.

Keir Starmer atakuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza huku chama chake cha Labour kikitarajiwa kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa bunge, matokeo ya awali yalionyesha Alhamisi, wakati chama cha Rishi Sunak kikitabiriwa kupata pigo kubwa la kihistoria.

Matokeo yameonyesha Labour kitashinda viti 410 katika bunge lenye viti 650 na wingi wa viti 170, na hivyo kumaliza miaka 14 ya serikali inayoongozwa na chama cha Conservative.

Chama cha Sunak kinatarajiwa kupata viti 131 tu, chini ya viti 346 wakati bunge lilipovunjwa, ni matokeo mabaya ya uchaguzi kwa chama hicho katika historia yake.

Wapiga kura wamekiadhibu chama hicho kutokana na mzozo wa gharama ya maisha na miaka ya ukosefu wa uthabiti na malumbano ya ndani ya chama ambayo yamepelekea Uingereza kuwa na mawaziri wakuu wa tano tangu 2016.

“Mustakabali wa Uingereza ulikuwa kwenye kura katika uchaguzi huu. Na ikiwa tumefanya vizuri usiku huu, Labour kitaanza kufanya kazi mara moja kwa kuchukua hatua za kwanza kwa ajili ya mabadiliko,” Pat McFadden, mratibu wa kampeni ya chama cha Labour alisema katika taarifa.

Forum

XS
SM
MD
LG