Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 18:50

Benki ya dunia yasimamisha kuipa mikopo Gabon


Kiongozi wa kijeshi wa Gabon Jenerali Brice Oligui Nguema
Kiongozi wa kijeshi wa Gabon Jenerali Brice Oligui Nguema

Benki ya dunia imesimamisha haki ya Gabon kupewa mikopo na ruzuku kuanzia Julai 1 kutokana na kushindwa kulipa madeni yake ya zamani, barua ambayo Reuters imeiona imethibitisha hilo Jumatano.

Taifa hilo la Afrika ya kati kwa sasa linalipa takriban mikopo 11 ya Benki ya dunia, kulingana na tovuti ya benki hiyo.

Benki ya dunia ilikubali kuikopesha au kuipa Gabon pesa ambazo sio deni, zaidi ya dola bilioni moja tangu mwaka 2012, na kutoa zaidi ya dola milioni 700.

Benki hiyo ilisema katika barua kwamba madeni ambayo hajalipwa ilikuwa karibu dola milioni 17 kufikia tarehe 30 Juni.

Msemaji wa Benki ya dunia alisema inasikitisha kuona barua rasmi imepenya na kufika kwa vyombo vya habari.

Kusimamisha kutoa pesa za mikopo ni utaratibu uliomo katika mikataba ya ufadhili, msemaji huyo alisema.

“Kuhusu Gabon, tuna imani kwamba mamlaka zitachukua hatua za kurekebisha hali hiyo haraka iwezekanavyo,” msemaji huyo alisema katika taarifa.

Miradi inayofadhiliwa na Benki ya dunia nchini Gabon ni pamoja na afya ya umma, ukuzaji wa ujuzi na takwimu, kulingana na tovuti ya benki ya dunia.

Wanajeshi walichukua madaraka nchini Gabon Agosti mwaka jana, na kumuondoa Rais Ali Bongo.

Forum

XS
SM
MD
LG