Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 30, 2024 Local time: 18:55

Maafisa wa Libya wafungwa jela kutokana na mkasa wa mafuriko


Uharibifu uliotokea kufutia mafuriko ya Derna, Libya. picha ya maktaba. Septemba 17, 2023.
Uharibifu uliotokea kufutia mafuriko ya Derna, Libya. picha ya maktaba. Septemba 17, 2023.

Mkuu wa sheria wa Libya amesema Jumapili kwamba mahakama imewafunga gerezani maafisa 12, kutokana na kuporomoka kwa mabwawa kadhaa mjini Derna, mwaka uliopita, ambapo maelfu ya wakazi walikufa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, maafisa hao waliotwikwa jukumu la kuendesha mabwawa nchini wamepewa vifungo vya kati ya miaka 9 hadi 27 gerezani, na mahakama ya rufaa ya Derna, wakati wanne miongoni mwao wakiachiliwa huru.

Derna, mji wa pwani wenye wakazi takriban 125,000, Septemba mwaka jana ulikumbwa na mafuriko mabaya yaliosababishwa na kimbunga Daniel. Maelfu ya wakazi walikufa baada ya mabwawa kuvunja kingo, huku wengine wengi wakitoweka. Mkuu huyo wa sheria kwenye serikali ya Tripoli amesema kuwa maafisa watatu miongoni mwa walioshitakiwa wameamurishwa kurejesha fedha walizopata kwa njia ya udanganyifu, kutokana na mkasa huo.

Ripoti ya Januari mwaka huu kutoka Benki ya Dunia, Umoja wa Mataifa na EU, ilisema kuwa mkasa huo ulisababisha janga la kimazingira linalohitaji dola bilioni 1.8 za kimarekani, kukarabati. Ripoti hiyo iliongeza kusema kwa kiasi fulani, mabwawa hayo yaliporomoka kutokana na udhaifu wa kiufundi, usimamizi mbaya, pamoja na matatizo ya kiutawala kufuatia ghasia za muda mrefu.

Forum

XS
SM
MD
LG