Mvua kubwa zimesababisha mafuriko yaliyojaza bwawa la Arbaat mnamo Jumapili, kilomita 40 kaskazini mwa Port Sudan, mji ambao sasa unatumika kama makao makuu ya serikali, wanadiplomasia, mashirika ya misaada na watu waliokoseshwa makazi kutokana na vita vya miezi kadhaa kati ya jeshi na kikosi cha kijeshi cha RSF.
Umoja wa Mataifa umesema kwamba karibu watu 50,000 wameathiriwa na mafuriko, na kwamba huenda idadi hiyo inajumuisha tu watu waliokuwa wanaishi magharibi mwa bwawa hilo na kwamba si rahisi kuwafikia watu walio mashariki mwa bwawa.
Bwawa hilo lilikuwa chanzo kikuu cha maji kwa ajili ya mji wa Port Sudan, unaokaliwa na watu wanaofanya shughuli zao kwenye bandari ya Bahari ya Shamu, na uwanja wa ndege, na kupokea misaada inayohitajika sana kwa ajili ya watu wa Sudan.
Timu ya serikali iliyoundwa kwa ajili ya kuthathmini athari ya mvua ilisema Jumatatu kwamba watu 132 wameuawa katika mfuriko kote Sudan na Umoja wa Mataifa umesema kwamba wengine 118,000 wamekoseshwa makazi.
Forum