Mvua kubwa Jumamosi zilisababisha mto mmoja karibu na mpaka wa China kuvunja kingo zake, na kupelekea hali ya hatari, shirika hilo la Korea Central News Agency, KCNA, limesema. Hata hivyo halikutaja idadi ya vifo wala kiasi cha uharibifu uliotokea.
Taarifa zimeongeza kusema kuwa helikopta 10 zilifanya safari kadhaa za kuwaokoa watu licha ya hali mbaya ya hewa, na hatimaye watu 4,200 walioathiriwa waliokolewa.
KCNA limemtaja Kim kuwa aliongoza shughuli za uokoaji Jumapili, wakati akiamuru upelekaji wa chakula pamoja na misaada mingine, kwa waathirika. Mafuriko ya msimu wa joto Korea Kaskazini mara nyingi husababisha uharibifu mkubwa kwenye mashamba kutokana na mifumo duni ya upelekaji ya mifereji ya maji, ukataji miti, na miundo mbinu dhaifu.
Forum