Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 15, 2024 Local time: 03:26

Watu 150 wapoteza maisha China kwa mmomonyoko wa ardhi


Maporomoko ya ardhi na mafuriko yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 150 kote nchini China katika miezi miwili iliyopita huku dhoruba za mvua zikiikumba eneo hilo.

Kazi ya kutafuta walioathirika iliendelea Jumatatu katika eneo la milima la Tibet katika mkoa wa Sichuan na kusababisha vifo vya watu 9 na wengine 18 hawajulikani waliko, vyombo vya habari vya serikali vimesema.

Maafa ya Jumamosi asubuhi yaliharibu nyumba na kuua takriban watu saba katika kijiji cha Ridi, shirika la utangazaji la CCTV limesema katika ripoti yake ya mtandaoni.

Watu wawili zaidi wamefariki dunia baada ya daraja lililokuwa karibu kati ya vichuguu viwili kuporomoka na magari manne kuporomoka.

China iko katikati ya msimu wake wa mafuriko, ambao unaanza katikati ya Julai hadi katikati ya Agosti, na watunga sera wa China wameonya mara kwa mara kwamba serikali inahitaji kuongeza maandalizi ya maafa kwa sababu hali mbaya ya hewa inazidi kuwa ya kawaida.

Forum

XS
SM
MD
LG