Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 02:07

Viongozi wa Florida, Georgia na South Carolina watangaza hali ya tahadhari


Hali ya barabara za Florida, Marekani kufuatia dhoruba ya Kimbunga Debby kikiathiri pwani ya Ghuba ya Florida.
Hali ya barabara za Florida, Marekani kufuatia dhoruba ya Kimbunga Debby kikiathiri pwani ya Ghuba ya Florida.

Watabiri wa hali ya hewa walitahadharisha Jumatatu kuhusu dhoruba ya  kimbunga inayotishia maisha, yenye viwango vya juu vya mvua na mafuriko yenye maangamizi katika eneo la kusini mashariki mwa Marekani wakati Kimbunga Debby kikiathiri pwani ya Ghuba ya Florida.

Kituo cha Taifa cha Kimbunga Marekani¸ NHC, kilisema kimbunga hicho kina kasi endelevu ya upepo wa kiasi cha kilomita 130 kwa saa mapema Jumatatu wakati kimbunga hicho kilipopiga karibu na Steinhatchee, Florida.

Kimbunga hicho kinaweza kuleta ufukweni wimbi kubwa la maji la hadi mita tatu zaidi ya mawimbi ya kawaida katika baadhi ya maeneo. Mawimbi yenye nguvu ni sababu kuu ya vifo kutokana na vimbunga, kulingana na NHC.

Baada ya kuleta athari Florida, kimbunga hicho kinatarajiwa kubakia katika kanda hiyo, kikielekea pole pole upande wa kaskazini na kuleta mvua kubwa Florida, Georgia na South Carolina katika siku zijazo.

Kimbunga Debby
Kimbunga Debby

Kiwango cha mvua cha sentimita 15-30 kinatarajiwa Florida, na sentimita 25- 50 huko Georgia na South Carolina. Magavana wa majimbo hayo matatu tayari wametangaza hali ya tahadhari kusaidia juhudi za misaada kuharakishwa.

Baadhi ya taarifa katika habari hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP na Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG