Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:03

Maelfu wakimbia dhoruba Bangladesh


Maelfu ya watu wa Bangladesh wameondoka katika vijiji vyao vya pwani Jumapili kwenda kwenye makazi salama kujikinga na dhoruba zaidi ndani ya nchi wakati taifa hilo likijiandaa kwa maafa yanayotarajiwa ya kimbunga kikali, maafisa wamesema.

Kimbunga Remal kilitarajiwa kuikumba nchi hiyo na sehemu za nchi jirani ya India Jumapili jioni, huku idara ya hali ya hewa ya Bangladesh ikitabiri mawimbi makubwa na upepo utakaovuma kwa kasi ya hadi kilomita 130 kwa saa.

Vimbunga vimeua maelfu ya watu Bangladesh katika miongo ya hivi karibuni, lakini idadi ya dhoruba zinazoikumba pwani yake ya nyanda za chini, yenye watu wengi imeongezeka sana hivi karibuni kutokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Kimbunga hicho kinaweza kusababisha mawimbi ya dhoruba ya hadi futi 12 juu ya mawimbi ya kawaida ambayo ni hatari, afisa mkuu wa idara ya hali ya hewa Muhammad Abul Kalam Mallik, ameambia AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG