Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:00

Kimbunga Beryl chasababisha vifo, uharibifu mkubwa wa mali Mexico


Kimbunga Beryl
Kimbunga Beryl

Kimbunga Beryl kilitua kwenye Peninsula ya Yucatan ya Mexico karibu na mji wa mapumziko wa Tulum kama dhoruba ya kiwango cha pili mapema Ijumaa, kikifagia miti na kusababisha kukatika kwa umeme, baada ya kusababisha  uharibifu, na vifo vya takriban  watu 11 kote Karibean.

Beryl kilitarajiwa kupungua kasi na kuwa dhoruba ya kitropiki wakati kikivuka peninsula hiyo kabla ya kuibuka tena katika Ghuba ya Mexico, na uwezekano wa kurejesha nguvu na kuwa kimbunga kikubwa tena, Kituo cha Kitaifa cha Vimbunga cha Merika kilisema.

Kimbunga hicho kilikuwa kimetabiriwa kuelekea kaskazini mwa Mexico karibu na mpaka wa Texas, eneo lililokumbwa na kimbuna Alberto wiki chache zilizopita.

Beryl ilisababisha uharibifu huko Jamaika, St. Vincent na Grenadines, na Barbados wiki hii baada ya kuwa dhoruba ya mapema zaidi kutokea na kuwa kimbunga cha Kitengo cha 5 katika Atlantiki.

Watu watatu wameripotiwa kufariki huko Grenada, watatu huko St. Vincent na Grenadines, watatu Venezuela na wawili Jamaica, maafisa walisema.

Forum

XS
SM
MD
LG