Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 15, 2024 Local time: 08:49

Ukraine yasema Russia imetumia droni, makombora ya masafa marefu katika mashambulizi ya usiku kucha


Mashambulizi ya usiku kucha ya ndege zisizo kuwa na rubani na makombora ya masafa marefu katika mkoa wa Odesa yaliyofanywa na jeshi la Russia usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu.
Mashambulizi ya usiku kucha ya ndege zisizo kuwa na rubani na makombora ya masafa marefu katika mkoa wa Odesa yaliyofanywa na jeshi la Russia usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu.

Ukraine ilisema Jumatatu kuwa Russia imetumia ndege 24 zisizo na rubani kushambulia mikoa ya Mykolaiv na Odesa usiku kucha, mbali na kufyatua makombora ya masafa marefu 17 kwa  Ukraine.

Jeshi la Ukraine lilisema limeangusha ndege 18 zisizo na rubani za Russia na makombora yote yaliyopigwa.

Oleh Kiper, gavana wa mkoa wa Odesa, alisema kuwa wilaya ya Izmail, ambayo ni eneo lililo na bandari zinazo safirisha nafaka, zilishambuliwa tena, na kituo cha michezo cha mji wa Vylkove kilishambuliwa pia. Hakuna ripoti zozote za vifo zilizotolewa.

Huko Mykolaiv, gavana wa mkoa huo Vitaliy Kim alisema kifusi kinachoanguka kilisababisha moto katika jengo hilo, huku wimbi la mlipuko lilisababisha uharibifu wa majengo mengine ya karibu.

Shambulizi la Russia katika mkoa wa Kherson lilijeruhi watu wasiopungua wanne, kulingana na gavana wa eneo Oleksandr Prokudin.

Prokudin alisema kuwa majeshi ya Russia yalifanya mashambulizi kwa makusudi katika eneo la kituo cha basi kilicho kuwa na watu wengi katika mji wa Beryl.

Naibu Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Hanna Maliar alisema Jumatatu kuwa majeshi ya Ukraine yalikuwa yamechuykua tena eneo la kilomita mbili za mraba kutoka kwa majeshi ya Russia katika eneo la Bakhmut, na pia zaidi ya kilomita za tano za mraba huko kusini mwa Ukraine.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii inatokana na mashirika ya habari ya The Associated Press, Agence France-Presse and Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG