Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 15, 2024 Local time: 10:43

Ukraine yakomboa vinu vya mafuta na gesi kwenye bahari ya Black Sea kutoka kwa Russia


Meli ya nafaka ya Ukraine ikiwa kwenye bahari ya Black Sea karibu na bandari ya Odesa. Picha ya maktaba.
Meli ya nafaka ya Ukraine ikiwa kwenye bahari ya Black Sea karibu na bandari ya Odesa. Picha ya maktaba.

Jeshi la Ukraine limesema kwamba limekomboa vinu vya mafuta na gesi kwenye bahari ya Black Sea kutoka mikononi mwa Russia, likieleza hatua hiyo kuwa muhimu katika kuchukua tena udhibiti wa Crimea.

Ripoti zinaongeza kuwa wapiganaji wa Ukraine wamepiga hatua kubwa kuelekea kukomboa Bakhmut, mji uliyozingirwa baada ya kuchukuliwa na Russia hapo Mei. Kwa kukomboa vinu hivyo Kyiv imepata nguvu zaidi kwenye vita vyake dhidi ya Russia.

Naibu waziri wa ulinzi wa Ukraine amesema kwamba wapiganaji wa Ukraine wamekomboa mji uliopo kwenye mkoa wa Donetsk wakati wakiendelea mbele, kuelekea kwenye miji mingine miwili kusini mwa Bakhmut.

Wakati huo huo Ujerumani imeahidi kuendelea kutoa msaada wa kijeshi, kifedha na kibinadamu kwa Ukraine, wakati ikitangaza kwamba msaada wake wa dola bilioni 23.6 ndio wa pili kwa ukubwa kwa taifa hilo, baada ya Marekani. Kufikia sasa wizara ya ulinzi ya Russia haijatoa tamko kuhusiana na taarifa hizo.

Forum

XS
SM
MD
LG