Akizungumza na shirika la habari la Reuters kwamba hali hiyo itategemea pia na kuwepo na mashambulizi machache ya meli za Russia.
Fedorov alisema utengenezaji wa ndege zisizo na rubani za Ukraine umeongezeka kwa zaidi ya mara 100 tangu mwaka jana.
Fedorov pia aliliambia Reuters kwamba Ukraine inafanyia majaribio mifumo ya teknolojia ya AI, ambayo inaweza kutambua shabaha kwa umbali umbali wa kilomita kadhaa, pamoja na vifaa vinavyoongoza ndege zisizo na rubani licha ya kuharibiwa nmitambo ya kivita ya kielektroniki.
Wakati huo huo, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza, katika taarifa zake za kijasusi za kila siku kuhusu Ukraine, ilisema kuna uwezekano kwamba Russia itaanza tena kutumia makombora ya masafa marefu ili kulenga miundombinu ya Ukraine wakati wa baridi.
Forum