Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 03, 2024 Local time: 20:15

Mataifa ya Caribbean yajitayarisha kwa ajili ya kimbunga Beryl


Mkazi afunga dirisha za nyumba yake kabla ya kimbunga Beryl kuwasili mjini Bridgetown, Barbados .Juni, 30, 2024.
Mkazi afunga dirisha za nyumba yake kabla ya kimbunga Beryl kuwasili mjini Bridgetown, Barbados .Juni, 30, 2024.

 Kimbunga kilichopewa jina Beryl kilikuwa kinakaribia kusini mashariki mwa Caribbean, wakati maafisa wa serikali wakiwasihi wakazi Jumapili jioni, kuchukua hifadhi ili kuepuka hatari zake, kilitarajiwa kuwa kwenye kiwango hatari cha tatu.

Kimbunga hicho kinatarajiwa kufika kwenye kisiwa cha Windward Jumatatu, wakati ilani ikitolewa Barbados, St. Lucia, Grenada, Tobago na St Vincent, pamoja na Grenadines.

Kituo cha kitaifa cha vimbunga cha Marekani chenye makao yake makuu huko Miami, kimetoa tahadhari kuwa kimbunga hicho ni hatari na chenye kutishia maisha. Beryl asubuhi ya Jumatatu kimeripotiwa kuwa umbali wa kilomita 175 kusini –kusini mashariki mwa Barbados, kikiwa na kasi ya upepo ya kilomita 195 kwa saa.

Kimbunga hicho kinatarajiwa kupita kusini mwa Barbados Jumatatu kikielekea kwenye bahari ya Caribbean na kisha Jamaica. Kinatarajiwa kupunguza kasi kufikia kati kati mwa wiki, ingawa kitabaki kuwa na nguvu ya kimbunga kikielekea Mexico.

Kimbunga Ivan cha 2004 ndicho cha mwisho chenye nguvu kukumba kusini mashariki mwa Caribbean, wakati kikifanya uharibifu mkubwa huko Grenada, kikiwa cha kiwango cha 3.

Forum

XS
SM
MD
LG