Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:15

Dhoruba yashambulia Texas na Oklahoma, Marekani


Dhoruba kali kote Texas na Oklahoma imeharibu nyumba na kituo cha usafiri wa barabara kuu ambako madereva walikimbilia kujificha, na kuacha maelfu ya watu bila umeme na uharibifu mkubwa Jumapili.

Afisa usalama amesema takriban watu watano wamekufa katika jamii moja ya Texas vijijini na wengi zaidi wamejeruhiwa.

Dhoruba hizo haribifu zilianza Jumamosi usiku na kujumuisha kimbunga ambacho kilipindua magari na kufunga barabara kuu karibu na jiji la Dallas.

Maafisa wamesema watu wengi walipelekwa hospitali kwa magari ya wagonjwa na helikopta katika kaunti ya Texas ya Denton, japo hawakufahamu mara moja kiwango kamili cha majeruhi.

Katika Kaunti jirani ya Cooke, afisa usalama Ray Sappington, ameiambia AP kwamba watu hao watano waliofariki ni pamoja na wanafamilia watatu waliopatikana katika nyumba moja karibu na Valley View, iliyopo mpakani na Oklahoma.

Forum

XS
SM
MD
LG