Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 00:01

India: Waokoaji Kerala wanatafuta manusura, 166 wafariki


Waokoaji wakiwa katika eneo la maporomoko ya ardhi huko Kerala, India.
Waokoaji wakiwa katika eneo la maporomoko ya ardhi huko Kerala, India.

Picha za video zilizochukuliwa kutumia ndege isiyokuwa na rubani imeonyesha wanajeshi pamoja na timu za uokozi wakipekuwa kwenye matope na mawe katika eneo la Kerala, India.

Wakati zoezi hili likiendelea mvua imeendelea kunyesha, wanatafuta manusura pamoja na miili ya watu waliokufa kwenye milima katika jimbo la Kerala nchini India, siku moja baada ya watu 165 kufa kutokana na maporomoko ya ardhi kufuatia mvua za masika.

Kufikia sasa karibu watu 1,000 wameokolewa kutoka kwenye vijiji vya milimani, na kwenye mashamba ya majani ya chai, katika mkoa wa Wayana na wengine 225 wakiwa hawajulikani walipo ripoti zimesema . Watu 166 wameripotiwa kufa na wengine 195 kujeruhiwa wakati televisheni ya ndani Asianet ikiripoti vifo 179.

Waokoaji wakiondoa miili ya waliofariki katika maporomoko ya ardhi huko Kerala, India.
Waokoaji wakiondoa miili ya waliofariki katika maporomoko ya ardhi huko Kerala, India.

Mvua kubwa kwenye jimbo la Kerala ambalo ni kivutio kikubwa zaidi cha watalii nchini India zilipelekea maporomoka ya ardhi Jumanne, na kusababisha matope pamoja na mawe kuanguka kuelekea sehemu za chini ambapo watu wengi walifunikwa na kufariki wakiwa wamelala.

Mkasa huo unasemekana kuwa mbaya zaidi jimboni humo tangu mafuriko ya 2018 yalipotokea ..

Forum

XS
SM
MD
LG