Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 04:25

Ndege zisizo na rubani zatumika kuwatafuta manusura wa maporomoko ya ardhi Ethiopia


Watu wakiwa katika eneo la wilaya ya Geze-Gofa lililoko kusini mwa Ethiopia lililokumbwa na maporomoko ya ardhi Julai 22, 2024. Picha na AFP
Watu wakiwa katika eneo la wilaya ya Geze-Gofa lililoko kusini mwa Ethiopia lililokumbwa na maporomoko ya ardhi Julai 22, 2024. Picha na AFP

Waokoaji wakisaidiwa na ndege zisizo na rubani, Jumatano walikuwa wakiendelea kuwatafuta manusura wa ajali iliyotokana na maporomoko ya ardhi yaliyoharibu wilaya ya kusini mwa Ethiopia, ambayo yamesababisha vifo vya watu 229 na kuathiri maelfu ya wengine.

Mashirika ya kibinadamu pia yalikuwa yakihangaika kuharakisha misaada ya dharura kwa jamii iliyokumbwa na maafa, tukio baya zaidi kama hilo kurekodiwa nchini Ethiopia, nchi ambayo inakumbwa na hatari kubwa ya majanga yanayohusiana na hali ya hewa.

Takriban watu 14,000 wanahitaji kuhamishwa kutoka wilaya hiyo kwa haraka, kwa sababu ya hatari ya uwezekano wa maporomoko zaidi ya ardhi, chanzo cha Umoja wa Mataifa kiliiambia AFP.

Wakazi wa wilaya hiyo wamekuwa wakichimba vilima vikubwa vya matope, kwa kutumia sepetu na mikono yao, kuwatafuta waathiriwa na walionusurika kutokana na maporomoko ya ardhi huko Kencho Shacha Gozdi, eneo ambalo ni ngumu kufikiwa katika jimbo la mkoa wa Ethiopia Kusini, mamia ya kilomita kutoka mji mkuu Addis Ababa.

Kufikia sasa, wanaume 148 na wanawake 81 wamethibitishwa kufariki katika janga hilo, lililokumba eneo la mbali na milima, Idara ya Masuala ya Mawasiliano ya Kanda ya Gofa ambayo inashughulikia eneo hilo, ilisema Jumanne.

Forum

XS
SM
MD
LG