Takriban watu 12 wamefariki na wengine 18 hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kunyesha iliyosababisha maporomoko ya ardhi mwishoni mwa wiki katika mgodi wa haramu wa dhahabu kwenye kisiwa cha Sulawesi nchini Indonesia, maafisa wamesema leo Jumatatu.
Maporomoko ya ardhi yalitokea Jumapili asubuhi katika wilaya ya Suwawa, kwenye jimbo la Gorontalo, yaliwaua wachimbaji na wakazi wanaoishi karibu na mgodi huo haramu, alisema Heriyanto, mkuu wa shirika la uokoaji la eneo hilo (Basarnas).
Watu watano walionusurika waliondolewa, alisema akiongeza kuwa kikosi cha uokoaji kilikuwa kinawatafuta watu 18 ambao hawajulikani waliko leo Jumatatu. Tumepeleka wafanyakazi 164, ikiwemo timu ya taifa ya uokoaji, polisi na wanajeshi, kuwatafuta watu waliopotea, Heriyanto alisema.
Forum