Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 21:37

Idadi ya vifo kutokana na poromoko la ardhi la Uganda yafikia 13


Timu za uokozi zikitafuta manusura kwenye poromoko la ardhi la Kiteezi jijini Kampala, Aug. 10, 2024.
Timu za uokozi zikitafuta manusura kwenye poromoko la ardhi la Kiteezi jijini Kampala, Aug. 10, 2024.

Polisi wa Uganda wamesema Jumapili kuwa idadi ya vifo kutokana na maporomoko ya ardhi kwenye eneo kubwa la kutupia taka mjini Kampala imefikia 13, wakati timu za uokozi zikiendelea kutafuta manusura.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, mvua kubwa ambazo zimekuwa zikinyesha katika wiki za karibuni zilisababisha kuporomoka kwa sehemu ya aneo hilo, ambalo ndilo pekee linalotumika kutupa takataka mjini humo, na kupelekea kufunikwa kwa baadhi ya nyumba zilizokuwa karibu, wakati wenyewe walipokuwa wamelala.

Mamlaka za jiji Jumamosi zilisema kuwa watu 8 walikufa, lakini kufikia leo idadi hiyo imeongezeka hadi 13, huku wengine 14 wakiokolewa. Shirika la Mslaba mwekundu nchini humo limesema kuwa mahema yamewekwa karibu na eneo la tukio, ili kutoa hifadhi kwa watu walioathiriwa.

Eneo hilo linalofahamika kama Kiteezi, kwa miongo mingi limekuwa likitupwa taka taka za Kampala, hadi kugeuka na kuwa mlima, huku wakazi waishio karibu wakilalamika kutokana na taka zenye sumu, pamoja na uharibifu wa mazingira.

Nchini Ethiopia, takriban watu 115 walikufa 2017 baada ya eneo la taka mjini Addis Ababa kuporomoka, huku wengine 17 wakifa 2018, mjini Maputo, Msumbiji, kwenye tukio sawa na hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG