Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 15:43

Maafisa polisi wapatao 100 kutoka Congo wamekimbilia Uganda


Bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC)
Bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC)

Maafisa hao waliwasili kupitia kivuko cha mpakani cha Ishasha wilaya ya Kanungu kusini magharibi mwa Uganda

Takribani maafisa polisi 100 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walikimbilia nchi jirani ya Uganda mwishoni mwa wiki wakati mapigano yalipoongezeka kati ya waasi wa M23 na jeshi huko mashariki mwa Congo, msemaji wa jeshi la Uganda alisema siku ya Jumatatu.

Maafisa hao waliwasili kupitia kivuko cha mpakani cha Ishasha wilaya ya Kanungu kusini magharibi mwa Uganda, alisema Meja Kiconco Tabaro, msemaji wa kikanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda.

Maafisa hao 98 waliwasili wakiwa na bunduki 43 na risasi na walinyang’anywa silaha zao. “walikuwa wanakimbia mapigano ya M23 pamoja na wanamgambo wengine na Jeshi la Congo, kuna ghasia nyingi huko na kisha kuna njaa pia,” alisema Tabaro.

Katika kipindi cha siku nne zilizopita, angalau raia 2,500 zaidi wakimbizi wa-Congo waliwasili Uganda wakikimbia ghasia zinazoendelea kwenye mpaka, alisema. “Sababu kuu iliyoshinikiza hatua hiyo ni kuongezeka kwa ghasia na ukosefu wa usalama”, Tabaro alisema akiongeza kuwa wanawake wajawazito, kina mama wanaonyonyesha na watoto wadogo ni miongoni mwa wakimbizi.

Forum

XS
SM
MD
LG