Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 16:56

Washukiwa wa jaribio la mapinduzi ya Sierra Leone wapewa vifungo virefu vya jela


Mji mkuu wa Sierra Leone. Freetown. Aprili 28, 2024
Mji mkuu wa Sierra Leone. Freetown. Aprili 28, 2024

Mahakama ya kijeshi ya Sierra Leone imetoa hukumu ya vifungo virefu vya jela kwa wanajeshi 24 kutokana na jaribio la kupindua serikali ya Rais Julius Maada Bio, Novemba mwaka uliopita.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, hukumu hiyo imetolewa Ijumaa jioni, wakati jaji akiwapa vigungo vya kati ya miaka 50 na 129. Wanajeshi hao ni miongoni mwa 27 waliofikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi kwa kushiriki kwenye jaribio hilo la mapinduzi ya Novemba 26, lililohusishwa mashambulizi ya bunduki dhidi ya kituo cha kijeshi, jela mbili pamoja na maeneo mengine, ambapo wafungwa 2,200 walitoroka, na zaidi ya watu 20 kufa.

Hukumu hiyo imefuata ile ya Julai ya raia 11, pamoja na afisa mmoja wa polisi na mmoja wa jela, wanaodaiwa kushiriki kwenye jaribio hilo pia. Kabla ya kutoa hukumu hiyo, Jaji Mark Ngegba, ambaye aliwahi kuwa afisa wa jeshi alisema kuwa, huku hiyo ni ya kutuma ujumbe kwa wengine kwamba tukio kama hilo halitastahimiliwa kamwe jeshini.

Familia za washukiwa hao zilisikika sikipiga mayowe muda mfupi baada ya hukumu zao kutolewa. Jaribio hilo lilitokea baada ya uchaguzi mkuu ambao Rais Bio, alishinda kwa muhula wa pili kwa kura chache. Ushindi wake ulilalamikiwa na chama kikuu cha upinzani cha APC, huku pia baadhi ya waangalizi wa ndani na wa kimataifa wakiutiliwa mashaka.

Forum

XS
SM
MD
LG