Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 04:15

Homa iitwayo Lassa yasababisha vifo Sierra Leone


Mkuu wa timu ya ikolojia James Koninga akiwa katika hospitali ya serikali ya Kenema June 12, 2024. Picha na JOHN WESSELS / AFP.
Mkuu wa timu ya ikolojia James Koninga akiwa katika hospitali ya serikali ya Kenema June 12, 2024. Picha na JOHN WESSELS / AFP.

Muongo mmoja baada ya janga la Ebola ambalo limeua zaidi ya watu 11,000 nchini Sierra Leone hivi sasa inakabiliwa na homa mbaya inayosababisha kifo inayoitwa Lassa. Virusi vinaambukizwa kwa njia ya binadamu kupitia panya ambao wanaugua.

“Leo, kuna kesi chache, lakini kiwango cha vifo kiko juu sana,” anasema Lassana Kanne, msimamizi katika hospitali ya serikali ya Kenema.

Sierra Leone tangu haijarekodi kesi za ebola tangu mlipuko ulipomalizika mwaka 2016, shukran kwa kiasi kutokana na chanjo.

Wilaya ya Kenema, ambacho ni kituo kikuu cha Ebola, wanasayansi wanatumia mafunzo waliyopata muongo mmoja uliopita kujaribu kusitisha kusambaa kwa homa ya Lassa.

Kwa ujumla kiwango cha vifo ni asilimia moja, Lassa haijakaribia kuwa ni ya kutisha kama Ebola, ambayo iliua takriban asilimia 50 ya wagonjwa, kwa mujibu wa shirika la afya duniani.

Lakini mtu mmoja kati ya watano waliokumbwa na Lassa wanakuwa na hali mbaya sana na kiwango cha vifo kiko katika asilimia 15.

Hakuna chanjo rasmi iliyopo na matibabu yake ni ya kiasi, huku makovu ya Ebola yakiwazuia wengi kwenda kutafuta msaada wa kuokoa maisha.

Lansana Kanneh, Msimamizi, Hospitali ya Serikali Kenema amesema

“Kabla ya kuzuka kwa Ebola kuzuka, tulikuwa tunapata idadi kubwa ya kesi, watu wengi walikuwa wanakuja hospitali wakiwa na homa ya Lassa na halafu wanarejea wakiwa katika hali mbaya zaidi”

“Lakini hivi sasa tunapata kesi chache tu za homa mbaya sana inayopelekea vifo. Moja ya sababu ni kwamba tumeona hizi kesi zikija katika hatua za mwisho kabisa, ambazo ni hatua mbaya sana. Kwahiyo wanapokuja wanakaa kama saa 24 au 48 katika hospitali na halafu wanafariki,” aliongeza.

Forum

XS
SM
MD
LG