Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 14:02

WHO: Mlipuko wa ugonjwa wa Marburg wamalizika Equatorial Guinea


Dkt Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika ya Shirika la Afya Duniani. (Photo courtesy of WHO)
Dkt Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika ya Shirika la Afya Duniani. (Photo courtesy of WHO)

Mlipuko wa ugonjwa hatari wa Marburg nchini Equatorial Guinea  umemalizika  kulingana na taarifa ya idara ya Afrika ya Shirika la Afya Duniani.

Idara hiyo ilitoa taarifa jana Alhamisi ikieleza hakuna mtu mwengine yeyote aliyeripotiwa kuambukizwa na virusi vya Marburg, siku 42 zilizopita baada ya mgonjwa wa mwisho kukamilisha matibabu yake.

virusi vya Ugonjwa wa Marburg vinafanana na vya Ebola.

Mlipuko wa ugonjwa huo ulitangazwa februari 13 na ilikua ni mara ya kwanza kutokea huko Equatorial Guinea.

WHO inasema kwamba Kulikua na watu 17 waloambukizwa na 12 walifariki.

Tangazo la kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa huo Equatoriual Guinea linafuatia tangazo kama hilo lililotolewa Tanzania wiki iliyopita.

Dalili za Marburg ni pamoja na homa kali, kichwa kuuma , uchovu mwingi , kutapika damu na kuharisha. Unatokana na virusi kama vya Ebola na uambukizwa kwa watu kwa njia ya popo.

Ingawa hakuna chanjo wala tiba ya anti-retroviral kwa ajili ya Marburg , WHO ilisema hivi karibuni juhudi zake za haraka kwa kutumia maafisa wa ndani na Serikali zimesaidia kuzuia ugonjwa huo kuenea.

Forum

XS
SM
MD
LG