Kesi tisa, ikiwemo vifo sita vimeandikishwa katika mlipuko huo ambao ulitangazwa mwezi Machi kaskazini magharibi mwa mkoa wa Kagera , WHO imesema.
Dalili za Marburg ni pamoja na homa kali, kichwa kuuma , uchovu mwingi , kutapika damu na kuharisha. Unatokana na virusi kama vya Ebola na uambukizwa kwa watu kwa njia ya popo.
Ingawa hakuna chanjo wala tiba ya anti-retroviral kwa ajili ya Marburg , WHO imesema juhudi zake za haraka kwa kutumia maafisa wa ndani na Serikali zimesaidia kuzuia ugonjwa huo kuenea.
Mkurugenzi mkuu wa WHO kwa Afrika Matshidiso Moeti amesema Tanzania imefanikiwa kutokomeza mlipuko wa ugonjwa huo na kuzuiya uwezekano wa matokeo mabaya ya ugonjwa huo unaoambukiza.
Forum