Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 03:40

Serikali ya Tanzania yachunguza ugonjwa usiojulikana ambao umeua watu 3


Ramani ya Tanzania
Ramani ya Tanzania

Serikali ya Tanzania ilipeleka timu ya madaktari na wataalamu wa afya kuchunguza ugonjwa usiojulikana ambao uliua watu watatu, serikali imesema Jumatano.

Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na homa, maumivu ya kichwa, uchovu na kutokwa na damu kwenye pua, daktari mkuu wa serikali Aifello Sichalwe amesema katika taarifa.

Kufikia sasa, visa 13 viliripotiwa katika mkoa wa kusini mashariki wa Lindi, mkiwemo watu watatu waliofariki.

Sichalwe amesema wagonjwa waliopimwa hawakuwa na Ebola na virusi vya Marburg, au Covid 19.

Amesema mmoja wa wagonjwa alipona , wengine wametengwa.

“Serikali iliunda timu ya wataalam ambao bado wanachunguza ugonjwa huo usiojulikana,” ameongeza, akitoa wito kwa wanainchi wa eneo hilo kuwa watulivu

XS
SM
MD
LG