Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 16:58

Ongezeko la idadi ya dharura za kiafya yalifanya Shirika la Afya Duniani 'kuelemewa’


Uharibifu uliosababishwa na mafuriko mjini Goma, DRC.
Uharibifu uliosababishwa na mafuriko mjini Goma, DRC.

Ongezeko la idadi ya dharura za kiafya kote  ulimwenguni, kuanzia COVID-19 hadi kipindupindu, imelifanya Shirika la Afya Duniani “kuelemewa” katika kukabiliana na hali hizo, mshauri wa ngazi ya juu alisema Jumanne.

Akiongea katika mkutano wa kila mwaka wa shirika la UN, Profesa Walid Ammar, mwenyekiti wa kamati inayotathmini hatua za dharura zinazochukuliwa na WHO, alisema kuna pengo katika ufadhili na wafanyakazi ambalo linaongezeka kutokana na mahitaji ya shirika hilo kuongezeka.

“Programu hizo zimeelemewa kutokana na mahitaji mengi kuongezeka na hali za dharura kusambaa na kuwa tete,” alisema.

Katika mwezi Machi, WHO ilikuwa inajibu jinsi ya kukabiliana na dharura za kiwango cha juu 53, ripoti ya kamati hiyo ilisema.

Hii ikiwemo magonjwa kama vile COVID-19, mlipuko wa kipindupindu na Marburg uliotokea huko Equatorial Guinea na Tanzania, na vilevilve dharura za kibinadamu kama vile tetemeko la ardhi nchini Uturuki na Syria na mafuriko nchini Pakistan.

Ripoti hiyo ilieleza kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yameongeza idadi ya matukio ya mafuriko na vimbunga, vyote hivyo vikiwa na athari za kiafya.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG