Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 08:30

Uganda yatangaza kumalizika kwa mlipuko wa Ebola


Waziri wa Afya wa Uganda Jane Ruth Aceng akipokea masanduku ya chanjo ya Ebola ya aina ya virusi vya Sudan, Entebbe, Uganda, Dec. 8, 2022.
Waziri wa Afya wa Uganda Jane Ruth Aceng akipokea masanduku ya chanjo ya Ebola ya aina ya virusi vya Sudan, Entebbe, Uganda, Dec. 8, 2022.

Uganda Jumatano imetangaza  kumalizika kwa mlipuko  wa  virusi vya Ebola, ambao ulilikumba taifa hilo miezi minne iliyopita na kuua  watu 55.

“ Tumefanikiwa kuudhibiti mlipuko wa Ebola nchini Uganda” amesema Waziri wa Afya Jane Ruth Aceng katika sherehe zilizofanyika katika wilaya ya kati ya Mubende mahali ambako ugonjwa uligunduliwa kwa mara ya kwanza mwezi Septemba.

Hatua hiyo imethibitishwa katika taarifa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambapo mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus alipongeza “majibu mazuri nay a kina” kukabiliana na ugonjwa huo ambao unasababisha homa na kuvuja damu.

Dr Aceng alisema Jaunuari 11, ni maadhimisho ya siku 113 tangu mlipuko ulipoanza ambao ulisambaa hadi mji mkuu wa Kampala.

Kwa vigezo vya WHO, mlipuko wa ugonjwa unaisha rasmi endapo hakuna visa vipya viliyoripotiwa kwa siku 42 mfululizo – mara mbili ya kipindi cha kuzaliana kwa virusi.

Uganda imetokomeza Ebola kwa haraka kwa kuweka hatua muhimu za kudhibiti maambukizi kama vile ufatiliaji, kuwafuatilia watu na maambukizi, kuzuia na kudhibiti,” taarifa hiyo ya WHO ilimnukuu waziri akisema.

“ Wakati tunaongeza jitihada zetu kuimarisha hatua madhubiti za kukabiliana na ugonjwa huo katika wilaya zote tisa zilizoathiriwa, nguzo yetu kubwa ni jamii yetu ambayo inaelewa umuhimu kufanya kilichohitajika kumaliza mlipuko wa ugonjwa huo, na kuchukua hatua.”

Chanzo cha habari hii kinatokana na gazeti la "The East African" linalochapishwa Kenya

XS
SM
MD
LG