Madaktari 15 wameambukizwa Ebola nchini Uganda na 6 wamefariki.
Uganda inakabiliana na mlipuko wa virusi vya Ebola aina ya Sudan ambayo haina chanjo.
Jumla ya watu 141 wamethibitishwa kuambukizwa Ebola na 55 wamefariki.
Shirika la afya duniani WHO na makundi mengine ya kutoa msaada yanaendelea kutoa msaada kwa Uganda kukabiliana na Ebola. Marekani imetoa msaada wad ola milioni 22 kupitia kwa washirika wake nchini Uganda.
Wizara ya afya ya Uganda imesema kwamba kuna uhaba wa wafanyakazi wa afya na vifaa kupambana na Ebola.