Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:12

WHO inasema kuwasili chanjo ya majaribio ya Ebola nchini Uganda ni ishara njema


Mfano wa chanjo ya majaribio ya virusi vya Ebola aina ya Sudan
Mfano wa chanjo ya majaribio ya virusi vya Ebola aina ya Sudan

Chanjo ya virusi vya Ebola aina ya Sudan ni moja kati ya chanjo tatu zilizopendekezwa kufanyiwa majaribio na jopo huru la wataalamu wa WHO. Chanjo nyingine mbili zitaongezwa kwenye majaribio wakati dozi zitakapowasili

Shirika la afya duniani (WHO) limesema kuwasili kwa moja ya chanjo tatu za majaribio ya Ebola nchini Uganda hapo alhamisi "kunaashiria hatua muhimu ya kihistoria katika uwezo wa kimataifa wa kukabiliana na milipuko".

Dozi 1,200 za chanjo ya virusi vya Ebola aina ya Sudan ziliwasili siku 79 tu baada ya mlipuko kutangazwa Septemba 20, WHO ilisema.

"Uganda inaonyesha kuwa utafiti wa kuokoa maisha unaweza kupangwa mara moja kati-kati ya mlipuko," alisema Dk Jane Ruth Aceng Acero, waziri wa afya wa Uganda.

Kwa upande mwingine, WHO ilisema kuwa "Kuanza majaribio ya Awamu 3 nchini Guinea wakati wa mlipuko wa Ebola huko Afrika Magharibi mwaka 2015, ilikuwa miezi 7 tangu kutangazwa kuwasili kwa chanjo. Haya yalikuwa mafanikio makubwa na kuweka rekodi za kihistoria wakati huo."

Chanjo ya virusi vya Ebola aina ya Sudan ni moja kati ya chanjo tatu zilizopendekezwa kufanyiwa majaribio na jopo huru la wataalamu wa WHO. Chanjo nyingine mbili zitaongezwa kwenye majaribio wakati dozi zitakapowasili.

XS
SM
MD
LG