Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 22:27

Maambukizi ya Ebola yanaendelea kusambaa Uganda


Watu wakiweka jeneza kwenye piki piki kwa ajili ya kusafirishwa kwa mazishi ya mtu aliyefariki dunia kutokana na maambukizi ya virusi vya Ebola katika wilaya ya Kassanda, Uganda. Nov 1, 2022
Watu wakiweka jeneza kwenye piki piki kwa ajili ya kusafirishwa kwa mazishi ya mtu aliyefariki dunia kutokana na maambukizi ya virusi vya Ebola katika wilaya ya Kassanda, Uganda. Nov 1, 2022

Wizara ya afya ya Uganda imetangaza kisa kingine cha maambukizi ya virusi vya Ebola katika wilaya ya Jinja, mashariki mwa nchi hiyo.

Waziri wa afya Jane Ruth Aceng amesema kwamba mwanamme mwenye umri wa miaka 45 alifariki alhamisi katika wilaya ya Jinja na vipimo vimethibitisha alikuwa ameambukizwa virusi vya Ebola.

Hii ni mara ya kwanza maambukizi ya ebola yanaripotiwa katika eneo jipya kutoka katikati mwa Uganda ambako mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza.

Maafisa wa afya wanaendelea kuimarisha mikakati ya kudhibiti maambukizi ya Ebola nchini Uganda tangu yaliporipotiwa mwezi Septemba tarehe 20.

Watu 135 wamethibitishwa kuambukizwa Ebola nchini Uganda, na 53 kati yao wamefariki dunia.

Hakuna chanjo dhidi ya virusi vya ebola aina ya Sudan, ambavyo vimeripotiwa nchini Uganda. Karibu nusu ya idadi ya wagonjwa wa Ebola hufariki dunia.

XS
SM
MD
LG