Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 07, 2024 Local time: 03:10

11 watiwa hatiani kwa jaribio la mapinduzi ya Sierra Leone


Mahakama ya Sierra Leone, Jumatatu iliwatia hatiani watu 11 kwa uhaini na makosa mengine kuhusiana na kile serekali inakiita jaribio la mapinduzi mwezi Novemba, msemaji wa mahakama amesema.

Mahakama ya Sierra Leone, Jumatatu iliwatia hatiani watu 11 kwa uhaini na makosa mengine kuhusiana na kile serekali inakiita jaribio la mapinduzi mwezi Novemba, msemaji wa mahakama amesema.

Amadu Koita Makalo, mwanajeshi wa zamani na mlinzi wa rais wa zamani Ernest Bai Koroma, amehukumiwa miaka 182 gerezani kwa makosa ya uhaini, mauaji na kumpiga risasi kwa nia ya kumuua, Elkass Sannoh, mkuu wa mawasiliano wa mahakama ameiambia AFP.

Koita Makalo alifuatiliwa sana kwenye mitandao ya kijamii ambapo aliikosoa serikali ya Rais wa sasa Julius Maada Bio, huku serikali hapo awali ikimtaja kuwa ni mmoja wa wanaopanga njama ya mapinduzi.

Wengine 10 pia walikutwa na hatia ya uhaini na mauaji, lakini haikueleza urefu wa vifungo vyao kwa kuwa hati ya mahakama ilikuwa haijatolewa.

Novemba 26 mwaka jana watu wenye silaha walivamia kambi mbili za jeshi, magereza mawili na vituo viwili vya polisi kujaribu mapinduzi.

Forum

XS
SM
MD
LG