Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 08:47

Watu 22 wafariki Sudan kufuatia shambulizi linalodaiwa kufanywa na RSF


Picha ya maktaba ya jeshi la Sudan.
Picha ya maktaba ya jeshi la Sudan.

Kundi moja la wanaharakati wa demokraisa nchini Sudan limesema Jumamosi kwamba tariban watu 22 wameuwawa baada ya kundi la kijeshi lenye silaha la Rapid Support Forces, RSF, kushambulia mji wa al-Fashir.

Kundi hilo la The al- Fashir Resistance Committee, kupitia ukurasa wake wa Facebook limesema kuwa wanamgambo wa RSF walirusha makombora kwenye soko, hospitali na makazi ya watu, na kwamba pia walitumia droni kulenga hospitali.

Mji huo ndio wa mwisho unaodhibitiwa na jeshi la serikali kwenye eneo la Darfur, ambalo ni ngome muhimu kwenye vita vyake dhidi ya RSF, ambavyo vimesababisha janga kubwa zaidi la kibinadamu duniani. Kundi hilo limeongeza kusema kuwa limehesabu miili 22, na kwamba idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Kufikia sasa hakuna tamko lolote kutoka kwa RSF, ambalo hapo nyuma limekuwa likikanusha kushambulia maeneo ya raia. Zaidi ya watu laki 3 wamelazimika kutoroka makwao huko al Fashir, kufuatia mapigano hayo, Umoja wa Mataifa umesema.

Forum

XS
SM
MD
LG