Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:25

Olympiki 2024: Marekani yaendeleza ushindi kwa kuifunga Sudan Kusini pointi 103-86


Mechi ya mpira wa kikapu wa wanaume Kundi C kati ya Marekani na Sudan Kusini, Paris, Ufaransa.
Mechi ya mpira wa kikapu wa wanaume Kundi C kati ya Marekani na Sudan Kusini, Paris, Ufaransa.

Marekani imeendeleza  kasi yake ya  ushindi kwa medali ya tano mfululizo ya dhahabu ya Olimpiki kwa ushindi wa  pointi 103-86 dhidi ya Sudan Kusini katika mchezo wa mpira wa kikapu wa wanaume,

Mashabiki wa Sudan Kusini wakionekana kuifagilia timu yao huko katika michuano ya Olimpiki ya mpira wa kikapu, Paris, Ufaransa.
Mashabiki wa Sudan Kusini wakionekana kuifagilia timu yao huko katika michuano ya Olimpiki ya mpira wa kikapu, Paris, Ufaransa.

Nayo Serbia iliilaza Puerto Rico kwa pointi 107-66 katika duru ya pili ya Kundi C katika mechi za Jumatano.

Sudan Kusini ikishiriki kwa mara ya kwanza, wakiongozwa na mchezaji wa NBA Royal Ivey, walikuwa wanatarajia kuishinda kwa mara ya saba Timu ya USA katika michezo ya Olimpiki na walionekana wakakamavu, wakitumia fursa kuwashinda Marekani kwa makosa yao ya awali wakati wa robo ya kwanza.

Haikuchukua muda mrefu kwa timu hiyo kurudi nyuma kutokana na urushaji mbovu wa mpira na makosa mfululizo na hivyo mabingwa walioongoza kwa pointi 19 wakati wa mapumziko.

Akiwa na mbwembwe kama kawaida na kuonekana amepata nafuu kutokana na jeraha, mshindi wa mara tatu wa Olimpiki Kevin Durant alionyesha uwezo wake wa ufungaji, akijipatia pointi 14 zikiwemo pointi 8 kati ya 9 zilizotokana na urushaji uliowaburudisha mashabiki katika uwanja wa michezo wa Pierre Mauroy.

Umati pia walikuwa wamefurahishwa na urushaji wa kustaajabisha wa Lebron James na Derrick White, walioweza kwa pamoja kupata pointi 22.

“Ilikuwa mchezo wenye nguvu, ninaheshimu jinsi (wachezaji wa Sudan Kusini) walivyocheza mechi hiyo,” alisema Durant.

“Historia ya Sudan Kusini inahamasisha, kile walichokifanya kama nchi, lazima uheshimu hilo,” aliongeza kusema Bam Adebayo wa Miami Heat, aliyeongoza timu ya Marekani kwa pointi 18.

Forum

XS
SM
MD
LG