Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 05, 2025 Local time: 06:09

Mtanzania ashinda nafasi ya Saba katika michuanao ya Paris Olimpiki


Collins Phillip Saliboko (mwenye kofia ya njano) wakati wa michuano ya kuogelea ya Olimpiki ya Paris, Julai 30 2024. Picha na Muhidini Issa Michuzi/ VOA
Collins Phillip Saliboko (mwenye kofia ya njano) wakati wa michuano ya kuogelea ya Olimpiki ya Paris, Julai 30 2024. Picha na Muhidini Issa Michuzi/ VOA

Tanzania imetupa karata yake ya pili siku ya Jumanne katika michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 wakati muogeleaji Collins Phillip Saliboko, alipoingia kwenye mashindano katika Olympic Aquatics Centre kitongoji St Dennis mjini Paris.

Katika michuano hiyo ya mita 100 (Freestyle) kwa wanaume Saliboko, alishika nafasi ya saba.

Saliboko nikijana anayechipukia katika kuogelea nchini Tanzania. alizaliwa wa katika mkoa wa Mbeya, ni muogeleaji aliyeonyesha ustadi mkubwa katika bwawa la kuogelea.

Akiwa na urefu wa sentimita 168 na uzito wa kilo 72, Collins ana sifa za kimwili zinazoakisi ujuzi, juhudi na kasi yake awapo majini.

Kujitoa kwake kwenye mchezo wa kuogelea kumemfanya kushiriki katika mashindano mengi ya kimataifa, akiiwakilisha Tanzania kwa fahari katika jukumu hilo gumu kutokana na upinzani mkali sana uliopo katika michezo ya kuogelea.

Forum

XS
SM
MD
LG