Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:52

Safari za treni za Ufaransa zarejeshwa tena baada ya mashambulizi


Picha ya maktaba ya treni za Ufaransa
Picha ya maktaba ya treni za Ufaransa

Treni 7 kati ya 10 za mwendo kasi za Ufaransa Jumamosi zimeanza tena safari zake, siku moja baada ya wahuni kuvuruga mfumo wa usafiri, wakati wa ufunguzi wa michezo ya Olimpiki mjini Paris.

Kufikia sasa hakuna kundi lililodai kuhusika kwenye uhalifu huo uliopangwa, wa mashambulizi ya kuchoma nyaya, usiku wa kuamkia Ijumaa. Uharibifu huo ulifanywa kwenye vituo mumimu vya treni, maeneo ya kaskazini, kusini magharibi na mashariki, zilizokuwa zikielekea kwenye hafla ya ufunguzi wa michezo hiyo mjini Paris, Ijumaa jioni.

Wafanyakazi wa reli wameripotiwa kuzuia jaribio la kuharibiwa kwa vifaa vingine vya kiusalama vya laini nyingine ya reli ambayo wamesema ingekuwa na athari kubwa. Kampuni ya reli ya Ufaransa ya SNCF, imesema kuwa treni za mwendo kasi za upande wa Kaskazini na Kusini Magharibi, zitaanza safari tena, japo kwa kuchelewa kwa muda wa saa moja au masaa mawili.

Taarifa zimeongeza kusema kuwa wafanyakazi wa reli wamefanya kazi usiku kucha, kwenye mazingira magumu, ili kurekebisha hali kwenye maeneo yalioshambuliwa.

Forum

XS
SM
MD
LG