Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 22:51

Olimpiki Paris: Mashirika ya Haki za Binadmau yaishutumu mamlaka ya Ufaransa kwa ukandamizaji


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kati) akizungumza na wanariadha wakati akitembelea eneo la uwanja wa mchezo"Stade Tour Eiffel" huko Champ-de-Mars mjini Paris, Ufaransa, 24 Julai 2024, kabla ya michezo ya Olimpiki Paris 2024 kuanza.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kati) akizungumza na wanariadha wakati akitembelea eneo la uwanja wa mchezo"Stade Tour Eiffel" huko Champ-de-Mars mjini Paris, Ufaransa, 24 Julai 2024, kabla ya michezo ya Olimpiki Paris 2024 kuanza.

Hatua hiyo pia imepelekea kudhoofisha ahadi za kufanya Michezo hii kuwa jumuishi zaidi kuwahi kutokea. Serikali inadai inajaribu kushughulikia tatizo la muda mrefu.

Mapema asubuhi watu wanahamishwa kutoka kwenye kambi ya wahamiaji kwenye ukingo wa Paris.

Wakazi wake hawajui nini kitakachotokea baadae.
Abdoulaye Sow, Mhamiaji kutoka Guinea anaeleza: “Walituambia tuje hapa, watatupatia makazi. Kutokana na Michezo ya Olimpiki, hatuwezi kubaki hapa. Watatuhamishia sehemu nyingine.”

Ufukuzaji wa aina hii si mpya. Makundi ya haki yamewakosoa hapo awali.

Lakini wanaharakati wanahoji ukubwa na muda wa kampeni hii ya hivi karibuni, imekuja kabla ya Michezo ya Olimpiki ya Paris.

Milou Borsotti wa Medecins Du Monde anaeleza: “Jinsi tunavyoelezea haya yote kwa sababu sio wiki hii tu; imeanza muda mrefu –tunauita ukandamizaji wa kijamii wa Paris. Kwa hivyo kimsingi kwa sababu ya Olimpiki, wana nia ya kuondoa taabu na umaskini wote mitaani”.

Shirika la hisani la Borsotti ni sehemu ya mtandao wa harakati, unaoitwa Other Side of the Medal . Unadai mamia ya watu wamehamishwa miezi kadhaa kabla ya Michezo.

Sio tu wahamiaji, wanasema pia Warumi, wafanyabiashara ya ngono na wengine wako kwenye shinikizo.

Ufunguzi wa michezo ya Olimpiki Paris 2024 mjini Paris, Ufaransa.
Ufunguzi wa michezo ya Olimpiki Paris 2024 mjini Paris, Ufaransa.

Baadhi ya wahamiaji wameripotiwa kupelekwa maeneo ya mbali na mji mkuu, wakipoteza kazi nzuri na kupata huduma za kijamii.

Mamlaka ya Ufaransa inasema wahamiaji wanaweza kuchagua wanakotaka kwenda

Adelyne Savy, Mkuu wa Wafanyakazi huko Ile de France: Tumekuwa tukifanya shughuli hizi kila wiki kwa miaka kadhaa zinatoa makazi katika eneo la Ile de France kwa watu wanaoishi katika mazingira magumu na yasiyo ya safi.

Pia tumepeleka watu mara kwa mara katika maeneo mengine ya Ufaransa, kwa sababu makazi ya dharura huko Paris yamejaa. Kwa hivyo tunapendekeza kwa watu ambao wamefika hivi karibuni bila mahusiano yoyote na Paris, kujaribu bahati yao mahali pengine.

Uhamisho huo unakuja huku kukiwa na ongezeko la hisia za kupinga uhamiaji nchini Ufaransa.

Inaongeza umaarufu wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally.

Jiji la Paris la mrengo wa kushoto linalaumu mamlaka ya kitaifa kwa kutowapa wahamiaji masuluhisho ya kutosha.
Lamia El Aaraje, Naibu Meya wa Paris anasema: Ni miezi kadhaa sasa ambapo tumeiomba serikali kuchukua udhibiti wa hali hii ambayo iko chini ya uwezo wao wa kipekee…

…Tunaendelea kuwapa wahamiaji maeneo kwa ajili ya makazi na misaada, lakini serikali inahitaji kuchukua majukumu yake.

Kwa sasa, wahamiaji hawa watapewa mahali pa kukaa karibu na Paris. Lakini pia wanaweza kurudi mitaani, wakati Michezo itakapomalizika.

((Lisa Bryant, VOA News, Paris))

Forum

XS
SM
MD
LG