Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekataa kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, akimuomba hii leo Jumatatu kuendelea kuwepo kwa muda kama kiongozi wa serikali baada ya matokeo ya uchaguzi yenye vurugu kuiacha serikali katika hali ya wasiwasi.
Wapiga kura wa Ufaransa waliligawa bunge katika mrengo wa kushoto, katikati na kulia, na hakuna kundi lolote litakalokaribia wingi wa kura zinazohitajika kuunda serikali. Matokeo kutoka kura ya Jumapili yameongeza hatari ya kupunguza kasi ya uchumi wa pili kwa ukubwa katika Umoja wa Ulaya.
Macron alisema uamuzi wake wa kuitisha uchaguzi mdogo utaipa Ufaransa “muda wa ufafanuzi”, lakini matokeo yalionyesha kinyume, chini ya wiki tatu kabla ya kuanza kwa michuano ya Paris Olimpiki, wakati nchi hiyo itakuwa katika jukwaa la kimataifa.
Forum