Rais wa Russia Vladimir Putin amewaonya washirika wa Ukraine, mataifa ya Magharibi, dhidi ya kutoa msaada wa vituo vya anga katika nchi zao.
Msururu wa mashambulizi ya anga mashariki mwa Syria Jumanne yaliua zaidi ya watu 10, akiwemo mshauri wa jeshi la Iran na mfanyakazi wa shirika la afya duniani (WHO), maafisa na ripoti zimesema.
Serikali ya Sudan Kusini Jumanne ilisema shule zitafunguliwa tena wiki ijayo baada ya kufungwa kwa wiki mbili kutokana na joto kali nchini kote.
Watu wanne walioshtakiwa kwa mauaji kwenye jumba la tamasha mjini Moscow wametambulishwa na mamlaka kama raia wa Tajikistan, baadhi ya maelfu ya watu wanaohamia Russia kila mwaka ni kutoka nchi hiyo maskini iliyokuwa mwanachama wa Umoja wa Kisovieti ili kutoroka maisha ya kubaguliwa.
Mwanamke wa kwanza kugombea urais kwenye uchaguzi wa Jumapili wa Senegal, huenda asipate ushindi, lakini wanaharakati wanasema kwamba kuwepo kwake kunasaidia kampeni ya muda mrefu ya kufikia usawa wa kijinsia kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi.
Raia wa Russia walianza kupiga kura leo Ijumaa katika uchaguzi wa rais wa siku tatu unaotarajiwa kumkabidhi kiongozi mwenye msimamo mkali Vladimir Putin muhula mwingine wa miaka sita huku mashambulizi mapya yakiendelea nchini Ukraine hadi katika eneo la Russia.
Mtandao wa TikTok kwa mara nyingine umejikuta katika hali tete baada ya wabunge wa Marekani kupitisha mswada ambao utapelekea mtandao huo kupigwa marufuku nchini kote Marekani.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump anaweza kujua leo ikiwa Mahakama ya Juu itamruhusu kushiriki katika uchaguzi mwaka 2024, wakati ambapo mgombea huyo mkuu wa chama cha Republican akiwa anakaribia katika uteuzi wa chama chake.
Raia wa Iran leo Ijumaa wameshiriki uchaguzi wa bunge na baraza kuu la viongozi wa dini huku kukiwa na hofu ya idadi ndogo ya watu ya wapiga kujitokeza na waconsevativu wakitarajiwa kuimarisha uongozi wao.
Baraza la Seneti la Ufaransa Jumatano liliidhinisha muswada wa sheria wa kuweka katika katiba ya nchi haki ya mwanamke kutoa mimba, na kuondoa kikwazo kikubwa kwa sheria iliyoahidiwa na Rais Emmanuel Macron ili kukabiliana na athari za hatua ya kubatilisha haki ya utoaji mimba Marekani.
Jaji wa mahakama ya rufaa ya New York, Jumatano alikataa ombi la Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kusitisha tozo ya faini ya dola milioni 454 katika kesi ya ulaghai dhidi yake, na kupinga ombi la mwanasiasa huyo kutaka aruhusiwe kutoa dhamana ya kiwango kidogo cha pesa anazodaiwa.
Mashambulizi ya Israel yalipiga kitongoji cha mji mkuu wa Syria Jumatano asubuhi, na kuua watu wawili na kusababisha uharibifu wa mali, kwa mujibu wa televisheni ya serikali ya Syria.
TikTok inachukua hatua kukabiliana na habari potofu kuhusu uchaguzi ujao wa Umoja wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na kuweka vituo vya kuhakiki taarifa ndani ya programu ya app yake, jukwaa hilo ambalo husambaza kanda za video lilisema Jumatano katika makala iliyochapishwa katika blogi yake.
Rais wa Russia Vladimir Putin amesaini sheria Jumatano ambayo itawawezesha maafisa wa usalama kutaifisha fedha, vitu vya thamani na rasilimali nyingine kwa watu waliokutikana na hatia ya kueneza “kwa makusudi taarifa potofu” kuhusu jeshi la nchi hiyo.
Vituo vya kupigia kura na wafanyakazi wa uchaguzi wanajitayarisha mjini Islamabad kabla ya uchaguzi wa bunge utakaofanyika hapo kesho Alhamisi.
Tuzo za 66 za Grammy zinafanyika Jumapili kwenye ukumbi wa Crypto.com mjini Los Angeles, California, Marekani, ambapo wanawake walitarajiwa kufanya vyema zaidi kuliko wanaume katika nafasi mbalimbali, kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya burudani.
Zaidi ya wahamiaji Warohingya 100 wametoroka kutoka katika kituo cha kizuizi nchini Malaysia baada ya maandamano, mtu mmoja akithibitishwa kupoteza maisha katika ajali ya barabarani, maafisa walisema Ijumaa.
Korea Kaskazini Ijumaa imeongeza uchokozi wa majaribio ya silaha kwa kufyatua makombora ya masafa marefu baharini, huku kiongozi Kim Jong Un akilitaka jeshi lake kufanya matayarisho ya vita wakati akitembelea kiwanda cha meli.
Maafisa wa uchaguzi wa Afrika Kusini wametembelea jela kote nchini , kama sehemu ya kuandikisha takriban wafungwa laki moja, ili washiriki kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2024.